Tathmini ya Mchango wa Vyombo vya Habari vya Kichina katika Kukuza na Kueneza Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image

Authors

Mwita, Marwa James

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chaukidu Press.

Abstract

Vyombo vya habari vya Kichina vimekuwapo katika eneo la Afrika Mashariki tangu miaka ya 1960. Redio China Kimataifa (CRI) ilianza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania mnamo Septemba 1961. Ili kupata wafanyakazi wa Kichina walio na uwezo wa Kiswahili, lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa kama somo katika Chuo cha Utangazaji cha Beijing. Hadi sasa idhaa ya Kiswahili ya CRI inatangaza katika lugha ya Kiswahili. Wasimamizi wengi wa idhaa hii ni Wachina na wanakimudu Kiswahili vilivyo. Katika miaka ya hivi karibuni, hususani kuanzia mwaka 2011, vyombo vya habari vya Kichina vinavyotangaza katika lugha ya Kiswahili vimeongezeka. Baadhi ya hivi vyombo ni Shirika la Habari la Xinhua (Kupitia runinga yake ya CNC mtandaoni), shirika la runinga la CCTV (mtandaoni) na kampuni ya usambazaji wa mawimbi ya StarTimes. Tangu ongezeko hili lishuhudiwe, hakujakuwapo na utafiti wa kuonesha ni kwa njia gani vyombo hivi vimechangia katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Makala hii ililenga kufafanua ni kwa njia gani vyombo vya habari vya Kichina vimechangia katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Ili kufanikisha lengo hili, mbinu mbalimbali za utafiti zilitumiwa. Makala mbalimbali zilisomwa na kuchanganuliwa kwa kina. Vilevile, vipindi na matangazo kadhaa yanayopeperushwa katika vyombo hivi yalichanganuliwa. Mwishowe, wafanyakazi wa baadhi ya vyombo hivi walihojiwa. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi.

Description

Makala hii inatathmini mchango wa vyombo vya habari vya Kichina katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki. Inajadili historia ya uwepo wa vyombo vya habari vya Kichina vinavyotumia Kiswahili, hususan Redio China Kimataifa (CRI), iliyoanza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania mwaka 1961. Aidha, makala inachunguza ongezeko la vyombo vingine vya habari vya Kichina vinavyotumia Kiswahili, vikiwemo Shirika la Habari la Xinhua, CCTV na StarTimes. Utafiti unachunguza namna vyombo hivi vinavyochangia katika ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili kupitia matangazo, vipindi na maudhui mbalimbali. Mbinu zilizotumika katika utafiti ni pamoja na mapitio ya maandiko, uchanganuzi wa vipindi na matangazo pamoja na mahojiano na wafanyakazi wa baadhi ya vyombo husika. Matokeo yanawasilishwa kwa njia ya ufafanuzi ili kubainisha nafasi ya vyombo vya habari vya Kichina katika kuimarisha matumizi, ukuaji na ueneaji wa Kiswahili kimataifa.

Citation

Mwita, J. M. (2023). Tathmini ya Mchango wa Vyombo vya Habari vya Kichina katika Kukuza na Kueneza Kiswahili. Chaukidu Press.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By